ROHO MTAKATIFU, MUNGU NDANI YETU

Wale ambao wamemkubali na kumpokea Yesu kama Mfalme na Mwokozi wao pia wamemkaribisha Roho wake mioyoni mwao.
“Mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”(Warumi 8:9).

Kwa hiyo hatuwezi kudai kuwa tuna Roho Mtakatifu ikiwa hatujamkaribisha na kumwacha akae ndani ya mioyo yetu.
“Hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe. »(1 Wakorintho 6:19)

Roho Mtakatifu anapokuja kukaa ndani ya mioyo yetu, hatuishi tena kwa kuufuata mwili, bali kuufuata roho. Anatupilia mbali mawazo yetu maovu na tabia za dhambi na kuzibadilisha na kupenda wema, kupenda ukweli na kuchukia dhambi.
Anatugeuza kuwa watu wapya na kutujalia karama zake mbalimbali (hekima, akili, ushauri, nguvu, sayansi, uchaji Mungu na hofu ya Mungu) ili kutuwezesha kufanya kazi zetu mbalimbali vizuri ndani ya Kanisa.
Hivyo, Roho Mtakatifu ni « Mungu ndani yetu ».
Je, uko tayari kuruhusu Mungu aishi moyoni mwako na kutawala maisha yako?

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kuiruhusu roho yako ije ikae ndani yetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI-RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *