Siku hizi, watu wanaodai kuwa watumishi wa Mungu huthubutu bila wasiwasi wowote au woga wowote, kuzifanya nyumba za Mungu kuwa nyumba za biashara.
Ni tabia ambayo Yesu haungi mkono.
Siku moja Yesu alienda Yerusalemu, « Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.”(Yohana 2:14-16)
Wale wanaothubutu “kuuza baraka”, huomba na kutoa unabii kwa watoto wa Mungu kwa ajili ya pesa, katika makanisa tofauti, hawana tofauti na wale waliofanya biashara haramu ya hekaluni.
Siku moja watachapwa viboko na kufukuzwa kutoka katika nyumba ya Mungu na mwenye makanisa yote, Yesu Kristo mwenyewe.
OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kuongozwa na Roho Mtakatifu daima ili tusiwafuate wale wanaopotea kutoka katika wito wao wa kweli katika makanisa yetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250 730 900 900
KIGALI – RWANDA