Mtume Paulo anatuambia mtazamo wa kuwa nao tunapoona wengine wakijikwaa:
« Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. »(Wagalatia 6:1)
Paulo hasemi hapa kuhusu watu wanaodumisha mifumo ya dhambi kimakusudi, bali kuhusu watu wanaojikwaa licha ya nia yao ya kuishi kwa utukufu wa Mungu.
Haya yanapotokea tusiwacheki, tusiwasambae wala kuwahukumu. Wala tusiwavumilie dhambi zao.
Bali, tunapaswa kuwarejesha kwa roho ya upole ili wasiumizwe.
Zaidi ya hayo, ni lazima tuwe waangalifu tusije tukaanguka katika dhambi sisi wenyewe au kufikiri kwamba sisi ni bora zaidi.
OMBI:
Bwana Mungu wetu, utusaidie kuwarudisha wale wanaojikwaa na kuona kwamba sisi pia tusiangukie dhambini.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA