Ikiwa una kiburi, unajiona kuwa juu sana na kujiinua juu ya wengine. Hili limeelezewa vyema katika Isaya 14:
« Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. »(Isaya 14:13-14)
Maneno haya yanamhusu mfalme wa Babeli, lakini kwa bahati mbaya, yanatumika pia kwa wengine wengi. Yanaelezea kiini cha kiburi cha mwanadamu.
Ni kiburi ambacho huwafanya wanadamu mara nyingi wafikiri kwamba wana majibu yote na kwamba wanaweza kuishi vizuri bila Mungu.
Ni upuuzi ulioje kujilinganisha na Aliye Juu!
Na bado, wakilinganishwa naye, wao ni “mavumbi kwenye mizani.”(ona Isaya 40:15)
Na tunapojilinganisha na wengine, je, nyakati nyingine hatujisikii bora na muhimu zaidi kuliko wenzetu, majirani zetu au watu fulani wa familia yetu? Hiyo ni kiburi.
Tujue kwamba « Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. »(Yakobo 4:6)
OMBI:
Mungu wetu wa milele, tujalie tuepuke roho ya kiburi maishani mwetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA