Kujigeuza ni mbinu ya watu wabaya ili watu wasiwatambue.
Hivi ndivyo ilivyo, miongoni mwa mambo mengine, ya mitume wa uwongo siku hizi ambao kwa kweli ni watendao kazi kwa hila au wahalifu zaidi.
« Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. »(2 Wakorintho 11:13-15).
Hata hivyo, hakuna maana ya kujigeuza kwa sababu, mara nyingi, katika hali fulani, Mungu huwafunulia watu wasiofaa ili kujidhihirisha kwao au kuwazuia na kuwalinda watoto wake.
Yeroboamu alipomtuma mkewe kwa nabii Ahiya, alimwambia kabla hajaenda:
« Ondoka, tafadhali, ujibadilishe, wasikujue kuwa mkewe Yeroboamu… »(1 Wafalme 14:1-3)
Biblia inatuambia kwamba Ahiya alipoisikia sauti ya miguu yake, akiingia mlangoni, alisema, « Karibu, mkewe Yeroboamu; mbona wajifanya kuwa mwingine… »(1 Wafalme 14:6)
Ni kweli, hakuna maana katika kujifanya kuwa mwingine.
Badala ya kujibadilisha, kila mtu afadhali aache uovu ambao anajulikana akuwe mtoto mwema wa Mungu.
OMBI:
Baba yetu aliye mbinguni, atusaidie tuwe watu wazuri kwelikweli.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA