Ishara na maajabu mengi yalipokuwa yakifanywa kati ya watu kwa mikono ya mitume, na idadi ya wale waliomwamini Yesu, wanaume kwa wanawake, iliongezeka zaidi na zaidi, wenye mamlaka walisimama kupigana nao.
Hapo ndipo Mfarisayo mmoja, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akawaambia,
« Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu. »(Matendo ya Mitume 5:38-39)
Basi hakuna maana ya kusimama kupigana na shauri au kazi ambayo unapuuza au kutilia shaka uhalisi, au uthabiti.
Ikiwa shauri au kazi yao kwa kweli haitoki kwa Mungu, bila shaka, itavunjwa au itajiangamiza yenyewe licha yao.
Lakini ikiwa inatoka kwa Mungu, hutafanikiwa kuiangamiza, hutweza kuivunja, kwa sababu utajikuta unapigana na Mungu.
Acha kupiga vita kazi za watu wengine.
OMBI:
Bwana Mungu wetu, utujalie kamwe tusithubutu kutaka kuharibu kazi za wengine.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA