HAKI SI KUTOKUA NA DHAMBI

Haki ni nini?
Haki ni kuwa na mtazamo sahihi kwa Mungu, uhuru kutoka kwa hatia na hukumu.
Hii haimaanishi kutokuwepo kwa dhambi, kwani « mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena. »(Mithali 24:16), na Biblia pia inatuambia kwamba « tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. »(1 Yohana 1:8)

Kwa kweli, mradi tuna mwili huu, mwili huu wa kufa, tunaweza kuanguka katika dhambi.
Lakini sisi (ambao tumemwamini Yesu na kumkaribisha katika maisha yetu kama Mfalme na mwokozi wetu) Mungu anatutambua kuwa wenye haki katika Yesu-Kristo.
« Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. »(Warumi 5:19)

Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii… »(Warumi 5:1-2)
Hata hivyo, si kwa sababu tu tuko chini ya neema ndipo tunaruhusiwa kutenda dhambi (Soma Warumi 6:15).
Tukianguka katika dhambi, lazima tuinuke na kuungama dhambi zetu, ili kurejesha uhusiano wetu sahihi na Mungu.

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utusaidie kuinuka daima na kuungama dhambi zetu kila tunapoanguka katika dhambi.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba.
Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *