Mtu anayepitia nyakati ngumu anaweza kufikiri kwamba huruma za Mungu zimeisha na rehema zake zimemkoma.
Na bado, ni uwongo.
“Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.”(Maombolezo 3:22-23).
Kwa kweli, wana wa Israeli wangeweza kusumbuka kuhusu wakati wao ujao kwa sababu mana ilitosha kwa kila siku na hapakuwa na chochote kilichosalia kwa siku iliyofuata.
Ingawa waliishi mkono kwa mdomo, kuokoka kwao kulihakikishiwa na Mungu, kwa sababu ya huruma yake kwao.
Sisi wana wa agano jipya lililotokea msalabani, hatuwezi kusumbuka maana tunaenenda katika huruma za milele zilizotoka kwa damu ya Yesu.
Ndiyo maana Yesu anatuambia:
“Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”(Mathayo 6:34).
Huruma tuzopewa zilimfanya Yesu asulubishwe na kufa msalabani, ambazo tunatembea juu yazo hadi leo, na zitatupeleka pia mbinguni, kwa sababu tulichagua kumfuata Yesu ambaye ni mwenye huruma kweli.
OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utupe kutumainia huruma zako.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA