Ingawa Shetani anatuibia kimwili na kiroho kile tulicho nacho, Biblia inatuhakikishia kwamba tunaweza kurejesha kila kitu ambacho shetani ametuibia.
Hizi ndizo hatua tano za kurudisha kile shetani ametuibia:
1. Kujua kwanza ni kwa njia gani tuliibiwa:
« Kumbuka ni wapi ulikoanguka, ukatubu… »(Ufunuo 2:5)
Mara nyingi Shetani hupitia dhambi ili kutuibia.
2. Kutubu:
Mara tu tunapotambua kwamba Shetani amepitia dhambi zetu ili kutuibia kilichokuwa chetu, ni lazima tutubu.
« Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe. »(Matendo 3:19)
3. Kuepuka kujichanganya na watu wa dunia:
Tunapojichanganya na watu wa ulimwengu, Shetani daima huchukua fursa hii ili kutunyang’anya kile tulicho nacho. Ni lazima tuepuke.
« Efraimu ajichanganya na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa. Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari. »(Hosea 7:8-9)
4. Kufahamu kwamba tuna uwezo juu ya shetani:
Kuunganishwa kwetu na Mungu kupitia Yesu hutupatia nguvu juu ya shetani.
“Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.”(Mathayo 18:18)
5. Kuomba:
Kupitia maombi tunaweza kumfanya shetani atapike kila alichokuwa amemeza.
« Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake. »(Ayubu 20:15)
OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kurudisha yote ambayo shetani ametuibia.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA