KAMA TAI !

Tai alionyeshwa katika nyakati za kale kuwa na uwezo wa kujitengeneza upya. Zaburi ya 103 ya Daudi inadokeza hili inaposema kwamba Mungu aturejeze kama tai.

« (Bwana) Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai. »(Zaburi 103:5)

Tai anapozeeka, hupoteza uwezo wake wa kuona, hawezi tena kuona mbali; anapoteza kusikia, hawezi tena kusikia kelele na ma sauti vizuri; anapoteza misumari yake, hawezi tena kuchukua mawindo yake na pia kupoteza nguvu zake, hawezi tena kuwinda na kuinua mawindo yake.
Ili kujirudishia nguvu, anawaacha wengine na kwenda kujitenga katika milima mirefu ambako anapoteza manyoya yake yote na kucha zake zote.
Anarudi tu kwa wengine baada ya kurudia upya, na manyoya mapya na misumari mpya. Anarudi akiwa amerejezwa.
Ni vivyo hivyo kwetu sisi: Nyakati zote tunazoweza kukutana nazo zinazotudhoofisha, zikimaliza nguvu na uwezo wetu, Mungu anaweza kutuokoa, kutuondoa, na tunaweza kutokea tena kwa watu wengine kama watu wapya, wenye nguvu zisizo za kawaida.
Tayari katika maisha yetu tunapokea kuzaliwa upya, kurejeshwa na Roho Mtakatifu. Ingawa utu wetu wa nje unaharibiwa kidogo kidogo, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku baada ya siku (2 Wakorintho 4:16).
Hivi ndivyo pia Mungu anavyowahuisha watoto wake kiroho.

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utujalie kuweka matumaini yetu kwako.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunakuomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

2 réponses sur “KAMA TAI !”

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *