MATESO HUUTANGULIA UTUKUFU

Je, unajua kwamba mateso hutangulia utukufu na ni sehemu ya mpango wa Mungu kwa maisha yetu?

Yesu anawaeleza wanafunzi wake wawili:
« Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? »(Luka 24:25-26)

Ilikuwa vigumu kwa wanafunzi hawa kuelewa kwamba utukufu wa Yesu ulitanguliwa na mateso.
Lakini hata katika Waebrania 2:9 tunasoma kwamba Yesu, “ kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima”.
Maumivu ya Yesu yalikuwa sehemu ya mpango wa Mungu. Ilikuwa ni lazima.

Hata hivyo, ukweli huu haumhusu Yesu pekee, unawahusu watoto wote wa Mungu.
Tungependa kushiriki katika utukufu wa Mungu, lakini hatupendi ukweli kwamba “imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.”(Matendo 14:22)
Ili tusikate tamaa na kuchanganyikiwa, ni lazima tuelewe kabisa kwamba mateso yanaweza pia kuwa sehemu ya mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
Tuwe wajasiri na kudumu katika imani.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, tusaidie kuelewa kwamba mateso ni sehemu ya mpango wako kwa maisha yetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *