MTU MCHA MUNGU AMEKUWAJE ?

Kuakisi moyo, hekima, na asili ya Mungu ndilo lengo la yeyote anayetafuta kuwa mcha Mungu.

Basi mtu mcha Mungu amekuwaje?
• Anatubu anapotenda dhambi (1 Yohana 1:9)
• Anajiona kuwa mfu kwa dhambi lakini yu hai kwa Mungu (Warumi 6:1-4, 11)
• Anatafuta kuwa mnyenyekevu kuliko kuinuliwa (Mithali 27:2)
• Anatafuta kuwa mtumishi badala ya kudai kutumikiwa (Marko 10:45)
• Anatafuta kujazwa na Roho Mtakatifu daima (Waefeso 5:18; Matendo 13:52; Wagalatia 5:25)
• Anatamani kumpendeza Bwana kuliko nafsi yake (2 Wakorintho 5:9)
• Anazaa matunda kwa ajili ya ufalme wa Mungu (Yohana 15:5-8)

Mtu anayemcha Mungu si mwanadamu mkamilifu, lakini anajitahidi kila siku kuiga maisha yake kulingana na Yesu.
Hatoi udhuru kwa dhambi na udhaifu anaoupata ndani yake, bali anamwomba Mungu kila mara msaada wa kuzishinda (Warumi 6:11-14).
Mtu yeyote anaweza kuwa mcha Mungu ikiwa anampenda Mungu kwa moyo wake wote na kutafuta kumtii katika maeneo yote ya maisha yake (Luka 10:27; Wagalatia 2:20).

Je! unataka kuwa mcha Mungu au wewe tayari ndiye?
Ikiwa wewe bado hujamcha Mungu, tafuta kuwa mcha Mungu ili kumpendeza Mungu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kuwa wacha Mungu kwa mioyo yetu yote.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *