NAMNA YA KUPIGA MAGOTI MBELE ZA MUNGU

Je, kweli tunampigia Mungu magoti kwa unyoofu?
Hapa kuna aina nne za magoti ya kupiga:

1. Kupiga magoti ya miili yetu
« Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta. »(Zaburi 109:24)
Tunapopiga magoti, mwili wetu wote unasimama mbele za Mungu, hii inaonekana kwa watu na kwa Mungu.

2. Kupiga magoti ya mioyo yetu
« Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. »(Mathayo 13:15)
Wakati moyo wetu ni wa kuasi, mwili wetu unaweza kuwa juu ya magoti yake bila moyo wetu kuwa.

3. Kupiga magoti ya mapenzi yetu
« Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. »(Luka 22:42)
Tunapiga magoti miili yetu na mioyo yetu mbele za Mungu, lakini kwa kukosa subira, tunaacha mapenzi yetu yatangulie kuliko ya Mungu.
Tukimwamini, mapenzi yake makamilifu yatakuwa yetu.

4. Kupiga magoti ya akili zetu
« Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote. »*(Mathayo 22:37)
Mawazo yetu yakipiga magoti kwa Mungu, inathibitisha kwamba tunampenda Mungu.

« Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. »(Zaburi 95:6)

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utujalie tupige magoti yetu yote mbele zako kwa unyofu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *