SIRI YA MAFANIKIO MAISHANI

Kuna njia ya maisha ambayo inaruhusu sisi kufanikiwa katika kila kitu tunachofanya. Huanza tunapopata shangwe yetu katika Neno la Mungu, kutafakari juu yake, na kuongozwa na kanuni zake.

« Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. »(Zaburi 1:1-2)

Zaburi hii inatufunulia kwamba tukienenda sawasawa na shauri la waovu hatuwezi kufanikiwa.
Kwa hakika watu waovu hutupatia ushauri mbaya ili tushindwe na hata kutuangamiza. Siku zote huwa na nia mbaya na wivu.
Pia inatufunulia kwamba ni lazima tuepuke kusimama na kuketi na wenye dhambi na wadhihaki wanaomdhihaki Yesu na wale wanaomfuata.
Kwa vile mito, maziwa na bahari ni mazingira mazuri kwa samaki, vilabu vya usiku, cabareti na mahali pengine ambapo watu wenye maadili ya kutiliwa shaka hupatikana mara nyingi, ni mazingira mazuri kwa dhambi, wenye dhambi na wakosaji. Ni lazima tuziepuke ikiwa tunataka kujulikana vizuri na kufanikiwa maishani.
Zaburi hii pia inatufunulia kwamba tukiamua kuliamini Neno la Mungu, kulitafakari siku baada ya siku, na kujiruhusu kuongozwa nalo, tutapata utulivu na kuzaa matunda. Sawa na mti uliopandwa kwa uthabiti unaozaa matunda kwa majira yake, Mungu atatumiminia baraka zake maishani mwetu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie daima tufurahie neno lako na kuongozwa nalo.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: +250 730 900 900
KIGALI-RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *