TUTUMIE UWEZO TULIOUPEWA !

Yesu Kristo hakuwahi kuwaombea wagonjwa walemavu na wafu, alitumia uwezo wake, akawaponya wagonjwa na walemavu yeye mwenyewe; na wafu akawafufua yeye mwenyewe.
Baada ya kufanya miujiza mingi, aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina:
« Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. »(Mathayo 10:1,8)

Ni uwezo huo ambao wanafunzi wake walitumia baada ya Yesu kurudi mbinguni.
Ni uwezo huo tulioupata pia tulipompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wetu.
Hata hivyo, hata pale tulipo na uwezo huu, hatuwezi kuutumia bila imani.
Yesu alisema tutafanya miujiza tukiwa na imani.
« Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. »(Luka 17:6)
Pia alisema:
« Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka… mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka. »(Mathayo 21:21)

Kwa hiyo tuwe na imani ya kuweza kutumia uwezo huu tulioupewa kwa neema ya Mungu.

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utupe imani ya kutumia uwezo wako uliotupa.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *