TUZINGATIE MAJINA ANAYOTUITA YESU

Tayari, mara tu tunapotokea,
Mungu anatuita KAZI YAKE:
« Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. »(Waefeso 2:10)

Tangu tunapokutana na mwanawe Yesu, Yesu anatuita RAFIKI zake:
« Ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. » (Yohana 15:15)

Tangu wakati tunapompokea maishani mwetu na kumkubali kuwa Bwana na Mwokozi wetu, Yesu sasa anatuita WANA WA MUNGU maana yake ni kaka na dada zake.
« Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. »(Wagalatia 3:26)

Baadaye, huyu Yesu tuliyempokea maishani mwetu anatubadilisha na kutuita KIUMBE KIPYA:
« Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. »(2 Wakorintho 5:17)

Hapa ndipo Roho Mtakatifu anapokuja kukaa ndani yetu na Yesu anaanza kuita miili yetu HEKALU:
« Hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe. »(1 Wakorintho 6:19)

Ikiwa baadaye tunajitolea kueneza neno la Mungu, Yesu anatuita sisi MASHAHIDI wake:
« Nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. »(Matendo 1:8)

Je, tunazingatia majina haya katika maisha yetu?
Hebu tuwe kwa dhati jinsi Yesu anavyotuita.

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utujalie daima kuzingatia majina haya ambayo Yesu anatuita na kutafuta kila wakati kuwa kama Yesu anavyotuita.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *