Biblia inatuambia kuhusu mtu anayeitwa Abramu ambaye alimtumaini Mungu licha ya hofu zake binafsi.
Bwana alimwambia Abramu, “Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.”(Mwanzo 12:1)
Je, ungetendaje ikiwa Mungu angekuomba uache nyumba yako, familia yako, starehe zako na mambo yote unayoyafahamu ili uende mahali usiyojulikana? Je, ungeogopa? Hii ndiyo changamoto ambayo Abramu alikabiliana nayo – na aliogopa, lakini Mungu akamwambia, « Usiogope. »(Mwanzo 15:1)
Mara nyingi, kwa ajili ya hofu, tunafanyia mambo machache sana Mungu, wengine, na sisi wenyewe.
Abramu ilimbidi aonyeshe imani na utii kwa Mungu, na kuweka woga wake kando. Kama Abramu angeinama kwa hofu, hangeingia katika hatima yake kuwa kile ambacho Mungu alimuumba kuwa – baba wa wingi wa mataifa.
Kujitoa kwenye hofu zetu kunabadilisha mpango wa Mungu kwa maisha yetu. Kwa hiyo fanya kile Mungu anachokuagiza ufanye…hata ikibidi ufanye kwa hofu! Kama Abramu, utaona kwamba thawabu ni kubwa.
OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utupe nguvu za kushinda woga wote.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA