Baadhi ya askari walinzi walipokwenda kwa makuhani wakuu kuwaambia kwamba Yesu amefufuka, wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, wakisema:
« Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. »(Mathayo 28:13)
Biblia inatuambia kwamba askari hawa walichukua pesa, wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.(Mathayo 28:15).
Je, ni nini nyuma ya njama hizi zinazoendelea hadi leo?
Ni ukweli kuhusu ufufuo wa Yesu ambao walikuwa hawataki ujulikane.
Hakika, ufufuo wa Yesu uliwaleta wanadamu wote katika agano jipya, ukiwaweka huru wanadamu kutoka katika kongwa la sheria na kuwaweka chini ya utawala wa neema ya Mungu.
“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”(Warumi 8:1-2)
Ukweli wa kifo na ufufuko wa Yesu ulishuhudia kwamba “tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.”(Waebrania 10:10)
Haya ndiyo mambo halisi ambayo makuhani wakuu hawakutaka watu wajue.
Walitaka watu wa Mungu waendelee kutoa dhabihu na matoleo kwa sababu ya hatia ya kuhukumiwa na kuadhibiwa na Mungu.
Hata hivyo, kupuuza neema ya Mungu na kuendelea kujisikia hatia ni kudhalilisha kazi ambayo Yesu alifanya msalabani.
OMBI:
Bwana Mungu wetu, utujalie kuelewa agano lako jipya pamoja nasi, lililotimizwa msalabani na Yesu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.
THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA