KUJITAMBUA

Maandiko yana mengi ya kusema kuhusu kujitambua.

2Wakorintho 13:5 inasema:
“Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.”

Daudi alijua kabisa kwamba Mungu alikuwa anatawala maisha yake, na alikuwa na imani kwamba Mungu angemkomboa kutokana na hatari iliyokuwa inakuja (1Samweli 17:37). Ndiyo maana hakumwogopa Goliathi.
Ikiwa tunafahamu kwamba Yesu Kristo yu ndani yetu, hatuogopi chochote.
Paulo alipokuwa akiwatesa Wakristo, Yesu alimwambia hivi: « Sauli, Sauli, mbona waniudhi? »
Akasema, « U nani wewe, Bwana? »
Naye akasema, « Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe ».(Matendo ya Mitume 9:5)
Yesu hakusema, « Kwa nini unawatesa hao wakristo au watu wangu? », alisema « mbona waniudhi? » kwa sababu ukimgusa mtoto wa Mungu, unamgusa Yesu mwenyewe.
Tujitambue, tufahamu kama kuwa Kristo yu ndani yetu, anayetushambulia au kutupiga vita anashambulia na anakipigana na Yesu mwenyewe tangu tumekuwa watoto wa Mungu.

OMBI:
Mungu wetu wa milele, utujalie kufahamu kwamba tunalindwa kwa sababu Yesu yu ndani yetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *