MAMBO SABA MUNGU ANAYOPENDA

Hapa kuna mambo saba ambayo Mungu anatamani kuona katika maisha yetu.

1. Mungu anataka tuwe wanyenyekevu.
“10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.” (Yakobo 4:10).

2. Mungu anataka tuzae matunda.
« …mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu. »(Wakolosai 1:10).

3. Mungu anataka tumtii na unyenyekevu wetu.
« Je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. »(1 Samweli 15:22)

4. Mungu anataka tumtegemee kabisa.
“Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu.”( Wafilipi 4:12-13 ) )

5. Mungu anataka tuwe na imani kwake.
“Pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”(Waebrania 11:6)

6. Mungu anataka tuwe watumishi.
« Sasa kwa kuwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, ninyi nanyi mnapaswa kuoshana miguu ninyi kwa ninyi. Nimewawekea kielelezo, ili mfanye kama mimi nilivyowatendea. Amin, nawaambia, hakuna mtumishi a mkuu kuliko bwana wake, wala mjumbe si mkuu kuliko yeye aliyemtuma.”(Yohana 13:14-16)

7. Mungu anataka tuwe waigaji wa mwanawe Yesu.
Mtume Paulo anatuambia hivi: “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.”(1 Wakorintho 11:1)

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie daima tuweze kufanya kile unachotaka.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *