NANI ANAYEDHIBITI MANENO YAKO?

Maneno sio maneno tu, ukweli ni kwamba maneno yana maana na nguvu. Na mojawapo ya nguvu kuu za neno lililonenwa ni uwezo wa kufichua hali ya ndani ya mioyo yetu.
Maneno yetu yanaweza kufichua ni kwa kiasi gani tumetiwa doa na kupotoshwa na ulimwengu au ni kwa kiasi gani tumegeuzwa kuwa sura na mfano wa Yesu Kristo.
Ndiyo maana Yakobo anasema:
« Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. »(Yakobo 1:26)

Ikiwa hatuwezi kudhibiti ndimi zetu na maneno yanayotoka katika vinywa vyetu yanafanana zaidi na ulimwengu kuliko Kristo, uchafu wa mioyo yetu unawekwa wazi.

Lakini ikiwa kweli tumo ndani ya Kristo, tu kiumbe kipya chenye moyo mpya na maneno mapya.
« Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. »(2 Wakorintho 5:17)
Ina maana kwamba tunavua utu wa kale na kuvaa utu mpya, na mojawapo ya njia tunazovua utu wa kale ni kuacha kuzungumza kama utu wa kale.

OMBI:
Mungu wetu wa milele, tusaidie kudhibiti maneno yetu na kuacha kuzungumza kama ulimwengu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *