HAKUNA KITU CHOCHOTE BILA MUNGU !

Baada ya kupokea utume wa kuwakomboa watu wa Israeli kutoka Misri, Musa alimwambia Mungu:

« Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. »(Kutoka 33:15)

Musa alitambua kwamba bila uwepo wa Mungu katikati yao, hawangefika mahali wanakoenda.
Hakika tukishindwa katika utume wetu, tusipofanikiwa majukumu yetu, tusipofanikiwa kutimiza ahadi zetu ni kwa sababu tunajituma bila kumshirikisha Mungu.
Tusifanye lolote tena bila kumshirikisha Mungu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie tusitembee bila uwepo wako kando yetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *