JE, KWELI UMEMCHAGUA YESU ?

Hata kama sisi ni wakristo, tukibatizwa katika maji mengi, hii haitoshi. Ni lazima tuwe tayari kuacha mambo fulani ili kumfuata Yesu kikamilifu, tuenende kwa imani na kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Mtume Paulo ambaye alifaulu kuacha kazi za giza za zamani zake anashuhudia jambo hili. Anasema:
« Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. »(Wafilipi 3:7)

Kwa kweli, maadamu hatujaachana na matendo ya giza, maadamu tunabaki kushikamana na mali za ulimwengu, na maadamu tunabaki watumwa wa dhambi, hatuwezi kudai kuwa tumemchagua Yesu.
Ni lazima kabisa tupige hatua, tuache na tukubali kwenda kule anakotuongoza Bwana Yesu.

Sasa wewe uliacha nini kwa ajili ya Yesu?

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, tupe nguvu ya kuachana na kila kitu kinachotuzuia kumfuata mwanao Yesu Kristo.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *