JE, MUNGU ANATOA USHUHUDA MZURI JUU YAKO ?

Baada ya Shetani kuzunguka-zunguka tu duniani na kutembea huku na huku humo, Mungu alimuuliza:
« Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. »(Ayubu 1:8)

Swali hili la Mungu kwa Shetani linaonyesha kwamba Mungu alijivunia Ayubu na alitoa ushuhuda mzuri juu yake.
Je! Na sisi pia anatushuhudia vizuri?
Je! Na sisi pia anatuona tukiwa wakamilifu na waelekevu?
Ni heshima kubwa kwa kila mwanadamu kutambuliwa na Mungu kuwa mkamilifu na mwelekevu.
Hebu basi na tutafute kumpendeza hadi pale anapofurahi kwamba sisi ni watoto wake wema.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie tuwe watoto wakupendezao.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *