JE, UNATAMBUA KAMA NI MUNGU ?

Daudi anaimarishwa na kumbukumbu za ukombozi ambazo Mungu amefanya zamani, na ambazo zimeripotiwa kwake na wazee. Kisha, anamwomba Mungu wa Yakobo ukombozi kwa ajili ya magumu anayopata.

« Maana sitautumainia upinde wangu, Wala upanga wangu hautaniokoa. Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu; Na watuchukiao umewaaibisha. Tumejisifia Mungu mchana kutwa, Na jina lako tutalishukuru milele.”(Zaburi 44:6-8)

Hebu tuwe, kama Daudi, na unyenyekevu wa kutosha wa kutambua kwamba Mungu ameingilia kati mara kadhaa na kutukomboa kutoka katika hali nyingi ngumu. Usiamini kwamba ni kwa nguvu zetu wenyewe, ushujaa wetu au hekima zetu.
Hebu tuangalie nyuma, tukumbuke hali zilizopita na kumwomba Roho Mtakatifu atuangazie, na atuonyeshe ukweli halisi uliotokea, tutatabua kama ni Mungu alituokoa, na tutaweza kuimarishwa ili kuweza kupita kwa ujasiri katika hali za baadaye ambazo hazitabiriki hadi sasa.

DUA:
Baba yetu uliye mbinguni, utusaidie kutambua kwamba ni Wewe unayetukomboa kutoka katika hali zote ngumu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *