MASWALI YETU YOTE LAZIMA YALISUDIE JINA LA YESU

Chochote kinachotuumiza au kutusumbua, lazima kiliinamie jina la Yesu!

Mtu mmoja wenye pepo alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu: « Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. »
Hata hivyo, kwa kuwa Yesu aliamuru pepo huyo kumwacha huyo, mara moja lilimwacha na kukimbia. Mtu huyo alipona mara moja na kupata fahamu zake.(Soma Luka 8:26-36)

Biblia inatuambia kwamba « Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi. »(Wafilipi 2:9-10).

Jina hili lina nguvu kwa sababu ni jina la yule aliyekufa kwa ajili yetu, aliyefufuka kutoka kwa wafu na ambaye leo yuko mkono wa kuume wa Mungu, kwa ajili yetu!
Ni jina lililo juu ya majina yote, na ambalo kila goti lazima lipigwe!

Ndio maana kila moja ya matatizo yetu, magonjwa, hata yale yanayotambulika kuwa hayatibiki kama vile saratani na ukimwi, changamoto kama vile umaskini, aibu na woga, lazima zianguke mbele ya Yesu kama yule mtu wenye pepo, ziiname wakisikia jina la Yesu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kuliitia jina la Yesu kila wakati katika hali ngumu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba.
Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *