TUWAOMBEE WENGINE

Je, unajua kwamba Mungu anaweza kufanya kazi kwa wema kwa ajili ya mtu kwa sababu ya maombi ya mwingine? Hii inaitwa « maombezi ».

Mfano wa kielelezo tunaupata katika kitabu cha Ayubu.
Baada ya Ayubu kukiri enzi kuu ya Mungu na kujinyenyekeza mbele zake, Mungu alizungumza na marafiki zake na Ayubu, Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi ili kuwakemea kwa maneno haya:
« Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. »(Ayubu 42:8)

Basi wakafanya kama alivyowaambia BWANA; na BWANA akakubali maombi ya Ayubu.
Tungefanya vyema kuwa na tabia inayosababisha watu (hasa wenye haki) kututakia mema na kutuombea. Mungu mwenyewe alianzisha mfumo huu wa kupitia mtu moja ili kubariki mwingine ili kuendeleza umoja. Maombezi ni tendo muhimu katika maisha ya Mkristo wa kweli kama tunavyoona pale na Ayubu ambaye ni lazima awaombee marafiki zake.
Yakobo 5:16 pia inatuambia:
« … ombeaneni mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu na yanafaa. »
Hiki ni kitia-moyo kwetu kuwa waadilifu mbele za Mungu, si kwa ajili yetu wenyewe bali pia kwa wengine ambao ni wanufaika wake.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie tukumbuke daima kuwaombea wengine.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©*
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: + 250 730 900 900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *