UHURU HALISI

“Kristo ametuweka huru,” mtume Paulo asema katika Wagalatia.

“Ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”(Wagalatia 5:13)

Baadhi ya watu waliogopa kwamba uhuru huo ungesababisha uasi-sheria na machafuko. Lakini Paulo anasema tusiitumie kujiingiza katika dhambi:
“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake… Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.”(Warumi 6:12-14).

Kuwa na uhuru katika Kristo kunamaanisha kutotii tamaa za dhambi. Tumewekwa huru kutokana na dhambi kwa sababu maadamu sisi ni watumwa wa dhambi, hatuwezi kumpenda na kumtumikia Mungu au watu wanaotuzunguka.

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utusaidie tuwe huru kutoka katika tamaa zetu za dhambi.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *