UKWELI NI MUHIMU

Mtume Paulo ambaye aliandika sehemu kubwa ya Agano Jipya, alijaribu kufikia kila mtu kwa injili, kwa sababu alitaka watu wapate ujuzi wa ukweli.(ona 1Timotheo 2:4).

Tunahitaji pia kujua ukweli na kuwaambia wengine, kwa sababu ni muhimu kwa maisha yetu.
Kwa nini ukweli ni muhimu?

① Ukweli hutuweka huru:
Yesu alisema, “Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.”(Yohana 8:32)

② Ukweli hutuongoza:
« Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote. »(Yohana 16:13)

③ Ukweli hutulinda:
‘Tunapopokea upendo wa ile kweli,’ tunajizatiti dhidi ya uwezo wa hila wa udanganyifu.(ona 2 Wathesalonike 2:10 na Mathayo 24:4)

OMBI:
Mungu wetu uliye mbinguni, tujalie tuijue ukweli na tuwaambie wengine.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *