USIWE MTUMWA!

Mungu alimtoa mwanae wa pekee msalabani ili kila mtu aweze kuwekwa huru kutoka katika utumwa wa uovu na dhambi.

« Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. »(Wagalatia 4:7)

Kwa nini basi wakristo wengi wanapenda kurudi katika hali ya utumwa?
Hakika watu wengi ni watumwa bila hata kujua.
Ingawa si watumwa wa dhambi tena, wamebaki au wamekuwa watumwa wa nadharia za kidini, itikadi za kisiasa, watumwa wa migawanyiko, au watumwa wa kiburi chao, na kadhalika.
Tunapaswa kuwa waangalifu ili tusiwe watumwa kwa njia yoyote ile, kwa sababu “tumenunuliwa kwa thamani”(1 Wakorintho 7:23).

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utusaidie tusiwe watumwa wa mtu yeyote au kitu chochote.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: +250 730 900 900
KIGALI-RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *