USIWEKE HARUFU YA MOTO

Biblia inatuambia kwamba marafiki wa Danieli yaani, Shadraka, Meshaki na Abednego, walitupwa ndani ya tanuru ya moto na kutoka nje bila kujeruhiwa “hata hawakusikia harufu ya moto.”
« …wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo. »(Danieli 3:27).

Ikiwa walitoka katika tanuru ya moto bila harufu ya moto, ni kwa sababu Mungu alikuwa pamoja nao katika moto na kuwalinda dhidi ya athari za moto huu.
Emanueli, jina la Yesu linamaanisha « Mungu pamoja nawe ».
Ikiwa sisi pia tunaishi na kutembea pamoja na Yesu, atadhihirisha na kuingilia kati wakati wa majaribu ambayo tutapitia. Hivyo tutatoka bila harufu yoyote ya moto wa majaribu.
Hakika wale ambao harufu ya moto wa mateso imewafikia, wanaendelea kushika harufu hii katika maisha yao baada ya msiba: Wana harufu ya kutoaminiana, hofu, chuki, kiwewe, uovu…
Lakini wale ambao Yesu amewalinda dhidi ya matokeo ya majaribu, hawana harufu yeyote.
Hata hivyo, Mungu anaweza kuwakomboa wale wanaoweka harufu ya moto wa majaribu mbalimbali katika nafsi zao kwa kueneza juu yao harufu ya ushindi wake, harufu ya upendo wake na wema wake kwao.(Soma 2 Wakorintho 2:14)
Wakati huo, majaribu yao yanakuwa ushuhuda wa utukufu wa Mungu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utulinde na matokeo ya majaribu mbalimbali tunayopitia.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☎: +250 730 900 900
KIGALI-RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *