JE, UMEWAHI KUKUTANA NAO ?

Watu ambao hawaelewi kwa nini unamtumaini Mungu na kwa nini unaomba wanakungoja katika nyakati ngumu za maisha yako ili wakucheke.

Biblia inasema kwamba « siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. »(2 Petro 3:3-4)

Je, umewahi kukutana nao?
Ikiwa bado haujakutana nao, fahamu kwamba itabidi kukutana nao.
Na ukikutana nao, usiwasikilize, usiwape nafasi ya kukuepusha na Mungu na kuharibu imani yako, dumu katika imani yako.
« Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. »(1 Wakorintho 16:13)

OMBI:
Bwana Mungu wetu, utupe nguvu ya kusimama imara katika imani yetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *