KWANINI UNAJISIFU ?

Huna sababu ya kujivunia jinsi ulivyo, kwa ulichonacho au kwa kile unachoweza kufanya.

« Una nini usichopokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? »(1 Wakorintho 4:7).

Maisha, uliyapokea,
Afya njema, umeipokea,
Utajiri ulio nao, umeupokea,
Maarifa na talanta ulizo nazo, umezipokea,
Familia na marafiki ulio nao, uliwapokea,
Fadhili na uzuri ambao wengine wanathamini kwako, umevipokea,
Na wokovu? Pia uliupokea kwa neema ya Mungu kama unawo.
Huna kitu, na wewe si kitu ambacho hukupokea kutoka kwa Mungu, acha kujisifu.
Kila kitu ni neema ya Mungu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie tusijisifu tena kwa vile tulivyo, tulivyo navyo na tunavyoweza kufanya.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *