NJIA ZIENDAZO SAYUNI ZIKO WAZI

Mtunga-zaburi anasema kwamba wale wanaomwamini Mungu na kumtumaini wana heri kwa sababu wanapata njia zilizo wazi mioyoni mwao:

« Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. »(Zaburi 84:5)

Kwa kweli, mioyo yetu bila imani katika Mungu ni jangwa lisilo na njia. Ni kuanzia pale tu tunapoifungua kwa Mungu, ndipo Roho Mtakatifu anafuatilia huko njia za imani na toba.
Kugundua njia ziendazo Sayuni kunamaanisha kwamba magumu yote yatashindwa mapema na imani iliyo moyoni mwetu.
Na ni nini kisichowezekana kwa moyo ambao nguvu zake ziko kwa Mungu? Hakuna kitu.
Kwa hiyo hakuna kitu kinachoweza kutuhangaisha ikiwa tunaweka utegemezo wetu kwa Mungu.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kuweka imani yetu yote kwako.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *