HAKUNA KITU CHA KAWAIDA, KILA KITU NI MUUJIZA !

Yesu alipoondoka kwenda kwenye Bahari ya Galilaya ili kukaa peke yake mahali pasipokuwa na watu, watu wengi walimfuata. Ilikuwa zaidi ya watu 5,000 na Yesu aliwafundisha mambo mengi.

Lakini, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, « akawaponya wagonjwa wao. »(Mathayo 14:14)
Pia aligawia makutano mikate mitano na samaki wawili na “wakala wote wakashiba.”(Mathayo 14:20)

Jambo la kushangaza ni kwamba wote walivutiwa na muujiza wa kuponywa kwa wagonjwa na ule wa kushiriki mikate na samaki pamoja na umati huu wa watu elfu tano, lakini hakuna mtu aliyeweza kutambua kwamba kuweza kusema na kusikika bila kipaza sauti kwa umati huu wa watu elfu tano pia ulikuwa muujiza mkubwa!
Watu hawa waliona ni jambo la kawaida kuongea na umati wa watu elfu tano na kujifanya wasikie, kama vile watu wa siku hizi wanaona ni jambo la kawaida kuwa hai, kuamka asubuhi baada ya kulala kwa muda mrefu, kuwa na afya njema, kula kutosha, kuona, kusikia, kusema, kufikiri, na kadhalika.
Na bado kila kitu, na hasa kile tunachokichukulia kama kawaida, ni muujiza.
Hakuna kitu cha kawaida, kila kitu ni muujiza!

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie kuona miujiza yako katika kila jambo na kukusifu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *