YASIYOWEZEKANA MWACHIE MUNGU

Hakuna aliyefungwa kwa lisilowezekana, lakini Mungu daima hufanya kazi katika lisilowezekana na anakataa kufanya kazi katika iwezekanavyo.
Yawezekanayo, Mungu anatuachia na kamwe hataki tufanye yasiyowezekana, kwa sababu anajua kwamba hatuwezi.

Bwana Yesu alipofika kwenye kaburi la Lazaro, ambaye alikuwa amekufa kwa siku nne, aliwaambia wanafunzi wake: “Liondoeni jiwe.”(Yohana 11:39)
Baada ya wanafunzi wake kuliondoa jiwe hili lililokuwa limewekwa mbele ya kaburi, Yesu akalia kwa sauti kuu: “Lazaro, njoo huku nje!”(Yohana 11:43)
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia: « Mfungueni… »(Yohana 11:44)

Basi kwa nini Yesu aliwaambia wanafunzi wake waliondoe jiwe na wamfungue Lazaro wakati yeye angeliweza kuamuru jiwe liondoke na sanda zifunguke?
Ni kwa urahisi kabisa kwa sababu Yesu anaacha yale yanayowezekana kwa watu kwa sababu Ye atunze yasiyowezekana.
Anasisitiza kabisa kwamba tufanye yote tunayoweza kujifanyia na kutunza yale ambayo hatuwezi kufanya.

OMBI:
Baba yetu uliye mbinguni, utujalie siku zote tufanye yote tuwezayo na kukuacha utufanyie yale yasiyowezekana kwetu.
Ni katika jina la thamani la mwanao Yesu Kristo tunaomba, Amina.

THE LION OF JUDAH MINISTRY IN THE WORLD©
thelionofjudahmission@gmail.com
☏: +250730900900
KIGALI – RWANDA

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *